Francis Cheka akikabidhiwa funguo za gari aliloshinda, anaemkabidhi ni Menya Jerry Slaa


Francis Cheka akikabidhiwa funguo za gari aliloshinda, anaemkabidhi ni Menya Jerry Slaa

Kama unakumbuka zaidi ya siku nne zilizopita kupitia millardayo.com kulikua na stori ya bondia Mada Maugo baada ya kushindwa kwenye pambano weekend iliyopita, kusema kwamba bondia mshindi ambae ni Cheka Francis alimtolea maneno aliyoamini kwamba alitaka kumfanyia ushirikina.

Maugo alisema baada ya stori kuzagaa kwamba Francis Cheka kapata ajali akiwa na gari alilozawadiwa huku ikidaiwa kamgonga muendesha pikipiki ambae alifariki dunia usiku wa hilo shindano, kuna vitu alivisikia kutoka mdomoni mwa Cheka na vilimfanya ahisi kulikua na chembechembe za uchawi.

Maugo alisema baada ya kwenda kumsalimia Cheka kwenye kituo cha polisi Osterbay, Cheka alimwambia “kama yule mtu wa pikipiki asingekufa basi wewe ndio ungekufa leo”

Ili kupata mambo yote kwenye usawa Francis Cheka amepatikana na kuamplfy kwamba “Maugo ni mropokaji na wala hakuja kuniona polisi baada ya hiyo ajali, mdomo wake ni mchafu ndio maana kafukuzwa kazi jeshini, mimi ni mwanamichezo, sio kweli na wala sipendi nimpige bondia mwenzangu afe”