WATOTO WAKIWA WAMESHIKILIA SILAHA ZA UANGAMIZAJI

WATOTO WAKIWA WAMESHIKILIA SILAHA ZA UANGAMIZAJI, SUDAN YA KUSINI

Jamhuri ya Sudan imekubaliana na mpango wa Muungano wa Afrika (AU) wa kusitisha uhasama na Sudan Kusini, lakini imesema itajilinda iwapo itashambuliwa.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilizipa muda nchi hizo mbili hadi Ijumaa kusitisha mapigano, la sivyo zitawekewa vikwazo .

Alhamisi, Sudan Kusini ilisema ndege za kivita za Sudan zilishambulia maeneo ya kijeshi katika jimbo la Unity, Sudan Kusini inasema pia ilishambuliwa ardhini.

BBC wameandika kwamba Serikali ya Khartoum haijasema lolote kuhusu shutuma hizo ambapo Kutokana na mpango wa amani wa Muungano wa Afrika ambao nchi hizo mbili zimeridhia, Sudan na Sudan Kusini pia zitatarajiwa kurudi katika meza ya mazungumzo katika siku chache zijazo.

Mzozo wa hivi karibuni ulianza mwezi uliopita wakati Sudan Kusini ilipodhibiti eneo linalodhaniwa kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta la hejlig, Japo Sudan ndio inayodhibiti eneo hilo kwa sasa, nchi hizo mbili bado zinaonekena kuwa huenda zikarejea vitani.