Rashidi-Yekini

Rashidi-Yekini kipindi akiwa kwenye Timu yake ya Taifa


Ni mchezaji aliyekuwa kati ya taifa ya Nigeria, ambaye alishawa hii kuwa mwanasoka bora mara mbili barania Africa.

aliziwa mwaka 1963 katika jimbo la KADUNA , na baadae alianza kucheza soka la kulipwa kwenye ligi Kuu Nchini Nigeria na badae alikwenda kuichezea klabu ya African Sports, Nchini Ivory coast, Na badae alikimbilia Nchini Ureno ambakoa alitoka na sifa ya kuwa Mfungaji magoli Hodari katika ligi ya daraja la kwanza ya Ureno ambapo Msimu wa 193-94 alikwa amesha funga magoli 34 katika mechi 32 alizocheza.

Kutokana na kuichezea timu ya taifa ya Nigeria msimu huo ambapo ilishiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Kombe la Dunia na baadae kufuatiwa na Kombe la Mataifa ya Afrika, alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 1993, akiwa mchezaji wa kwanza wa Nigeria kupata tuzo hiyo.

Rashid Yekini, ambaye alikuwa ametalikiana na mkewe tangu mwaka 1994 alikuwa akiishi maisha ya tabu na wapangaji wengine wachahe katika nyumba yake mjini Ibadan, jimbo la Oyo ambapo iliarifiwa mara chache sana alikuwa akitembelewa na wageni.

Yekini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48 kutokana na ugonjwa wa akili na alikuwa baba wa watoto wawili, atazikwa Jumamosi kwa mujibu wa taratibu za dini ya Kiislamu huko Irah, jimbo la Kwara.