Sajuki

Picha ya kwanza kushoto ni Sajuki kabla ya kuugua, ya pili ni hali yake ya sasa, picha ya tatu ni ya Wastara

Wastara ambae ni Mke wa mwigizaji wa movie za kitanzania SAJUKI akiwa mgonjwa sasa hivi, amethibitisha kwamba pesa zisizopungua laki nane za kitanzania nimeibiwa kwenye account yake ya simu ya mkononi aliyokua anaitumia kupokelea pesa za msaada wa watanzania kumsaidia Sajuki kwenda kutibiwa.

Wastara ameiambia millardayo.com kwamba “ni kweli msg zilikua ni nyingi sana na kabla ya kuingia kwenye kipindi cha Leo tena CLOUDS FM kilichoendesha zoezi la kuchangia, simu ilikua ina pesa kidogo lakini cha ajabu nikaja kukuta hela ni ndogo kuliko msg zilizokuwepo pia baada ya hapo msg zikagoma kuendelea kuingia”

“kwa haraka haraka pesa iliyochukuliwa ni zaidi ya laki nane, na tulichokifanya tumemuomba mkurugenzi aiblock hiyo namba ili tuone kama zimeshatolewa au bado na ninategemea kwenda kwenye ofisi zao wakala manake hii sio mara ya kwanza kuibiwa, nilishawahi kuitangaza namba kupitia CLOUDS FM siku moja lakini siku ya pili tu zikaibiwa pesa zote ambazo ni laki nne, nilifatilia lakini mwisho wa siku akaja kulipa wakala wenyewe wenye shirika wakasema hawahusiki”

Mpaka sasa bado Wastara anaendelea kumtafuta mtu alieweza ku-hack simu yake na kuzimiliki hizo pesa ambazo anatumiwa kwa njia ya simu ya mkononi, millardayo.com inaendelea kufatilia…. kama kutakua na chochote cha ziada utafahamu kupitia hapahapa.

Source:MILLARD AYO