Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julis Nyerere, Dar es Salaam

Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julis Nyerere, Dar es Salaam

Polisi walimkamata mwanamke wakizambia akiwa amemeza vidonge vya madawa ya kulevya aina ya Heroine na kumlazimisha ambaye aliweza kutoa vidonge 49 ambayo vinathamani ya 1 milioni ya kizambia ambayo ni sawa sawa na Laki 3 za kitanzania

Jina la mwanamke huyo anaitwa Mary Mvula, ambaye alimeza vidonge hivyo na kujiadai ni mjamzito iliaweze kupita kwenye mipaka ya nchi, alikamatwa kwenye uwanja wandege wa Mwalimu Nyerere tarehe 2, may 2012.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa anarudi Zambia kutokea Pakistan kupitia Dubai.

Godffrey Nzowa, ambaye ni kaimu kamishina wa kuzuia madawa ya kulevya aliongea kwenye vyombo vya habari kuwa walimplisha Mary Mavula matunda ilikulainisha choo ili aweze kutoa vidonge vya madawa ya kulevya, ila hakusema ni matunda waliompa ale.

Nzowa alisema Mary hakuweza kwenda chooni kwa siku tatu baada ya kukamatwa , ingawa walimpa hayo matunda kuongeza spidi ya kupata choo.

Mkuu wa polisi alisema Mvula mwishoni aliweza kupata choo na kuweza kutoa vidonge 49 vya heroine, jumamosi baada ya kuka siku tatu bila kutoa kidonge hata kimoja.

Alisema kuwa Mtuhumiwa bado amebakiwa na vidonge vingi ambavyo viko tumboni na bado wanaendelea kumpa hayo matunda ili aweze kutoa hizo heroine nyingi zilizobakiwa,

Nzowa alisema mara ya kwanza Mvula alidanganya ana ujauzito ili aweze kukwepa kipimo cha X-ray lakini polisi waligundua kuwa sio mjamzito.

Alisema Mvula anakaa Lusaka na Passport namba yake ni ZN 190899 iliyotole mnamo taehe 10 octoba 2010. alisema Mvula atapelekwa mahakamani baada ya upelelezi kutoka.

Source:Zambian Watchdog