Lulu akiwa anaelekea Mahakamani

Lulu akiwa anaelekea Mahakamani

UTATA kuhusu umri wa mtuhumiwa wa kesi ya mauaji, mwigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo umeanza kutoa matokeo, kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, huku kesi yake ikipigwa tena kalenda hadi Mei 21, mwaka huu.

Lulu kwa sasa anasema ana umri wa miaka 17, lakini kabla ya kifo cha Kanumba alisema kwenye kipindi cha Mkasi Eatv kwamba ana umri wa miaka 18.

Wakili wa Lulu Kennedy Fungamtama leo aliwasilisha ombi Mahakamani akiitaka iitupilie mbali kesi hiyo ili ikafunguliwe upya katika Mahakama ya Watoto, akidai Lulu ana umri chini ya miaka 18.

Lakini Wakili Mwandamizi wa Serikali, Elizabeth Kaganda alipinga akisema suala hilo, inabidi kwanza lifanyiwe uchunguzi na vyombo vya dola ili kugundua ukweli kuhusu umri wa Lulu.

Tayari msisimko wa kesi hiyo unaonekana kuanza kupungua taratibu, kwani leo Lulu aliwasilishwa katika ulinzi wa kawaida mahakamani na hakukuwa na idadi kubwa ya watu kama ilivyokuwa mara ya pili mwezi uliopita.

Source:mamapipiro.blogspot.com