Libya

Maafisa wawili wa usalama nchiniLibya wameuawa baada ya waasi wa zamani kushambulia ofisi ya Waziri Mkuu mjini Tripoli ambapo Mtu aliyeshudia alisema magari aina ya pick-up yaliyobeba makombora yalilizunguka jengo hilo na mapigano yakaanza.

BBC wameandika kwamba Msemaji wa serikali baadaye alisema mapigano yamekwisha lakini Mashambulizi yanaarifiwa kufanywa na waasi wa zamani waliopigana kumuondoa madarakani Kanali Gaddafi mwaka uliopita ambao wanadai malipo yao waliyoahidiwa kupewa kwa utaratibu wa maalum.

Watu wengi waliokuwemo katika jengo hilo walikimbia akiwemo Waziri wa Fedha na Naibu Waziri Mkuu ambapo mshauri wa habari wa waziri mkuu Ashur Shamis aliiambia BBC kuwa waziri mkuu na maafisa kadhaa walikuwa salama na kwamba mapigano hayo yaliyodumu kwa saa kadhaa, yalikwisha.

Walioshuhudia walisema mashambulizi yalifanywa na wanamgambo kutoka Yafran, mji uliojaa wafuasi wa kundi la kikabila la Berber lililo umbali wa kilometa 100 (maili 60 ) kusini magharibi mwaTripoli lakini bado haijulikani Waziri mkuu Abdurrahim al-Keib aliko mpaka sasa.

Afisa mmoja wa wizara ya ndani alisema takriban askari wawili wa usalama waliuawa na wengine kujeruhiwa katika mapigano hayo huku mwandishi wa BBC Rana Jawad mjini Tripoli akisema pamoja na kupatiwa fedha, waasi hao wanadai wale waliojeruhiwa wakati wa mapinduzi mwaka jana wamepewe matibabu nje ya nchi.

Mpango wa malipo ulisitishwa mwezi uliopita huku kukiwa na tuhuma za udanganyifu na hii ikiripotiwa kuwa sio mara ya kwanza kwa kushambuliwa, hili ni la pili katika kipindi cha miezi miwili, lakini mara hii kuna nguvu zaidi ambapo Serikali ya Libya imekuwa ikijaribu kuwashawishi mamia ya wanamgambo walioshika silaha dhidi ya Kanali Gaddafi kuzisalimisha huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama.

Source: millardayo.com