Tanzania ipo kwenye mkakati wa kutengeneza na kuongeza ajira ndani ya miaka mitano ijayo, ni miongoni mwanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kutokana na report iliyotolewa na kampuni ya kimataifa ya Consultation Ernst & Young. Inaonysha kuwa miaka mitano inayokuja jumuiya ya Africa Mashariki itaweza kuongeza na kutengeza ajira 56,300 ambazo zitatengenezwa na wawekezaji kutoka nje.

Tanzania ndio nchi itakayo ongeza ajira kwa wingi zaidi kuliko nyingine kwa asilimia 49 ambazo ni sawa na ajira 28000, ikifuatia Kenya ambayo itaongeza ajira 16000, kutokana na repoti hiyo.
Repoti hiyo inasema ongezakaji wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni yaani foreign direct investments (FDIs), kiuchumi itaweza kupunguza tatizo la ajira , pia kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu. Kati Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Uganda na Rwanda wateweza kutengeneza na kuongeza ajira 11000 na watetengeza ajira hizo kwa mtiririko wa ajira 1300. The Ernst & Young’s 2012 Africa Attractiveness Survey Building Bridges inaonyesha kuwa madini, gesi na mafuta yaliyopo yanaendelea kuwavutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza na kutengeneza ajira.

Kutokana na mafuta yaliyo yaliyogunduliwa kaskazini mwa Kenya karibu na ziwa Turkana mafuta hayo yaliguduliwa na kampuni ya Tullow. Na kutokana na mazingira mazuri ya biashara nchi Rwanda , Madini na Mafuta yaliyopo Uganda yatatafanya kuvutia watu wengi kuwekeza kutoka nje.
Pia, ni kanda ya vivutio vingine ni pamoja na kiwango cha chini cha ukiritimba, mgawanyiko njia nzuri za kiuchumi kama vile mawasiliano, huduma za kifedha na utulivu wa kisiasa katika nchi ya Tanzania.
“Tanzania inayotarajiwa kuwa ni moja ya nchi ambazo uchumi wake utaongezeka kwa kasi ulimwenguni ,kwa sababu ya utulivu wa kisisa uliopo,” sehemu ya repoti ilivyoandikwa.
Uwekezaji Tanzania umekuwa ukikukuwa kuanzia kipindi cha mwaka 2003 mpaka Mwaka 2011, ambapo Tanzania iliweza kutengeneza dola za kimerekani Bilioni 13.2 zilizowekezwa na wawekezaji

“Pamoja uwekezaji Nchini Kenya kuwa duni, sehemu kubwa ya uwekezaji wa nguvu kazi imekimbilia kwenye sekta nyingine kama sekta ya mawasilano” inabainisha ripoti
Hata hivyo, Kenya ambayo imeingia kwenye uwekezaji wa moja kwa moja wa wageni “FDIs” inatarajia kutengeneza dola za kimerakani dola 1.3 bilioni kutokana na mafuta yaliyo gundulika Kenya na kampuni ya Tullow.