Hivi karibuni Samsung wamekuja juu kama watengenezaji na wauzaji wakubwa wa simu, wakiwa mojawapo ya kampuni zinazouza zaidi simu za kisasa ‘smart phones’.
Ni moja ya kampuni zinazoangaliwa zaidi katika ulimwengu wa Android. Kwa kutangaza ujio wa simu mpya, mashabiki wa simu inabidi wakae mkao wa kula.

Samsung Galaxy S III

Samsung Galaxy S III: Sura ya mbele

Samsung Galaxy S III

Samsung Galaxy S III: Sura ya Nyuma

Samsung Galaxy S III ni simu mpya inayoutumia teknologia ya kisasa na ikiwa ina Android ‘OS’, inajumuisha ‘quad-core processor’, ‘4.8″ 720p HD skirini’ na 8MP kamera, yenye urefu wa 8.6mm.

Inatumia ‘Ice Cream Sandwich’ ikiwa ni skirini ya kushika (touch screen) ikiwa ina mitindo mipya na mizuri ya kuitumia. Ina S Voice (inashinda na Siri ya iPhone),
eye-tracking(Smart Stay) ambayo itazima mwanga wa skrini endapo utakuwa umefumba macho au umelala na vingine vingi vizuri. Inatarajia kutoka Mei 29

Samsung Galaxy S III

Inatarajiwa kuachiwa kwenye masoko ya simu hadi Mei 29, kwa sasa watu wanaweza kuweka oda kwa bei ya kama 1,268,600 TShs (pound 499.95)

Kwa kuangalia sifa zake unaweza ukahamasika zaidi na kuona hii ni simu sahihi ya kutumia kwa kipindi hiki, lakini bado kuna simu nyingi kali na za kuvutia kama HTC One X (jina jingine mnyama ‘The Beast’). S III inahitaji kuwa bora zaidi kuweza kuwapiku washindani wake, tutaendelea kuwaletea habari zaidi kuhusu Samsung Galaxy S III.

Source: GSM Arena