Hilda & Julio, waliiwakilisha Tanzania Big Brother 2012.

Baada ya wawakilishi wote wa Tanzania kutolewa kwenye jumba la Big Brother Afrika, Hilda na Julio.. imefahamika kwamba ni kura chache sana zilizomfanya mshiriki wa Zimbabwe kubaki kwenye jumba hilo japokua nae alikua kwenye hatari ya kutoka.

Katika Exclusive na Millard Ayo wa AMPLIFAYA Clouds Fm, Hilda amesema “jamani najisikia vibaya kweli, unajua ukiwa na watu wanaokupenda wanaofurahi kwamba umefika ulipofika alafu unatolewa bila kutarajia inauma kuliko hata ungetolewa labda ukiwa unachukiwa na mtu fulani, au mtu flani hataki niwe kwenye nyumba, hii imekua tofauti kwa sababu mashine imeamua tutoke”

Amesema “imefika sehemu lazima tukubali na sasa hivi kila wiki kati ya watu wanne watakua wanatoa watu, wanne ndio anabaki na kuingia Up Ville ambapo ndio kuna kina Prezzo huko kwa hiyo nafikiri kutakua na watu kama kumi na nne ambao watajumuika na mastaa alafu ndio nafikiri mfumo wa kawaida ndio utaendelea japo hatujui itakuaje”

Alipoulizwa na millardayo.com kama kuna uhalali wa yeye kutolewa, Hilda amesema “sidhani kama ni halali kwa sababu nafikiri mimi nilikua mmoja kati ya wachezaji wazuri kwenye nyumba, pia naweza kusema Mzimbabwe ambae amebaki kwenye nyumba amenipita tu kwa kura mbili, kama ningepata watanzania wawili wanipigie kura kabla ya jana asubuhi saa kumi na mbili kuna uwezekano tungekua wote ndani ya nyumba sasa hivi, nimepitwa na kura mbili tu yeye alipata kura nane, mimi sita alafu wengine ndio wanafata… najua ningepata hizo kura mbili na nyie mngekua mnakula bata sasa hivi kupitia Tv nisingewaangusha, lakini namshukuru Mungu kwa kweli nataka niwaambie Asante sana”

Source:millardayo.com