NAHODHA wa Bayern Munich, Philipp Lahm amesema ni lazima waifunge Chelsea hapo kesho kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa kama wanataka kuwa miongoni mwa ‘kizazi cha dhahabu’ cha klabu hiyo.

Bayern watawakaribisha Chelsea jijini Munich kwenye Uwanja wa Allianz Arena wakati vijana hao wa Bavaria wakiwa na hamu ya kupata taji la kwanza tangu 2001, huku wakiwa wamecheza fainali mbili kati ya tatu zilizopita.

Lahm alikuwemo kwenye kikosi cha Bayern kilichofungwa 2-0 na Jose Mourinho akiwa na Inter Milan mwaka 2010 katika fainali ya Madrid.

Rais wa sasa wa Uli Hoeness na mwenyekiti Karl-Heinz Rummenigge, walikuwa kwenye kikosi cha Bayern kilichotwaa taji hilo mara tatu mfululizo mwaka 1974, 1975 na 1976.

Lahm atawaongoza wenzake kesho katika kuhakikisha wanategeneza historia ya kulitwaa taji Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili na mara ya tano pamoja na lilivyokuwa Kombe la Ulaya.

“Unahitaji kutwaa mataji ya kimataifa kama unataka kuingia kwenye rekodi za kizazi cha dhahabu,” alisema beki huyo mwenye miaka 28.

“Unatakiwa kunyakuwa ubingwa wakati unapoingia kwenye fainali. Ni wazi ni fajara kutwaa ubingwa. Sina miaka mingi ya kuendelea kuwa katika kiwango cha juu.”

Bayern wakiwa na majeraha ya kuchapwa 5-2 na Borussia Dortmund Jumamosi iliyopita katika fainali ya Kombe la Ujerumani na kocha Hoeness amewatadharisha nyota wake kuwa mabingwa wa Kombe la FA, Chelsea ni hatari zaidi.

“Chelsea imeimalika zaidi kwa sasa, kwa sababu hawakuwa na msimu mzuri katika ligi,” alisema.

“Kama wakifungwa katika fainali, hawatoshiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao na wote tunajua nini kitatokea kwa timu kama Chelsea.

“Kwa yeyote anayefikiri kuwa tayari tumeshashinda mechi hiyo atakuwa anafanya kosa kubwa.”

Bayern wanataka kuwa timu ya kwanza baada ya Inter iliyotwaa ubingwa kwenye uwanja wake wa San Siro mwaka1965.

“Wachezaji wengi waliokuwa kwenye kikosi chetu kwa sasa ni wale waliocheza fainali ya 2010,” alisema Lahm.

“Tumekuwa na kupata uzoefu zaidi. Hamu ya kutwaa ubingwa ni kubwa zaidi sasa kuliko ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.”

Akiwa mtoto muokota mipira katika fainali ya Ligi ya Mabingwa iliyochezwa Munich mwaka 1997, Lahm alikiri kuwa hakuwahi kuota siku moja atakuwa nahodha wa Bayern katika fainali ya Ulaya.

“Wakati ule sikuwa hata na ndoto kuwa siku moja nitakuwa nishindania taji kwenye jiji hili,” Lahm alilimbia gazeti la Munich iitwalo Sueddeutsche Zeitung.

Nahodha huyo wa Ujerumani na Bayern, alikuwa na miaka 13, wakati Dortmund ilipotwaa ubingwa kwa kushinda 3-1 dhidi yar Juventus mwezi Mei 28, 1997 kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini Munich.

Uwanja wa Munich waAllianz Arena wenye kuchukua watu 69,000, tangu mwaka 2005 umekuwa uwanja wa nyumbani wa Bayern tiketi zote zimeuzwa kwa mechi hiyo ya kesho, lakini fainali hiyo pia itashudiwa kwenye uwanja wa Olimpiki ambako maelfu ya mashabiki wameshanunua tiketi kwa lengo la kuangalia mechi hiyo kwenye Televisheni kubwa hapo

Source:MWANANCHI