Club ya soka ya Liverpool imethibitisha kwamba haina haraka ya kumtafuta kocha mwingine atakaeziba nafasi ya Kenny Daglish alietimuliwa jana, ila watahakikisha kwamba atakaechaguliwa kuwa meneja wa club hiyo atakua ndio bora kuliko wengine wote.

Club hiyo ilishinda kombe moja msimu huu uliopita ambapo ilitoa taarifa za kushtua kuhusu kukatisha mkataba na daglish jumatano, miezi 16 tu tangu aanze kuifundisha.

Sky sports wameandika Ingawa aliiwezesha club hiyo kushinda kombe la carling na kuifikisha Liverpool kwenye fainali za FA, matokeo mabaya kwenye ligi ya uingereza yamemgharimu Kenny daglish kwenye kazi yake.

Wamiliki wa club hiyo tayari wameanza harakati za kumtafuta atakaechukua nafasi ya Kenny Daglish ambapo pia mkurugenzi wa club hiyo Ian Ayre ameapa kwamba zoezi hilo litachukua muda wowote utakao hitajika hadi watakapopata kocha anahitajika kuirudisha Liverpool kwenye line.