Flaviana Matata akikabidhi Life Jackets (picha kutoka kwa Maria Tseshai )

Mwanamitindo mtanzania Flaviana Matata ametoa life Jackets mia tano (500) na kuzikabidhi kwa mamlaka ya bandari Mwanza (TPA) kama kumbukumbu ya miaka kumi na sita ya ajali ya meli ya MV BUKOBA.

Flaviana amesema “nimetoa hizo life Jackets kwa ziwa Victoria ambapo ajali hiyo ndipo ilipotokea ambapo mama yangu alikua mmoja wa waliofariki dunia”

Flaviana Matata mwenye makazi yake London U.K na New York Marekani anakofanya kazi, amesema alitoka na hizo Life Jackets nje ya nchi baada ya kuzioda kiwandani na angependa watanzania wenye uwezo wa kufanya hivyo wafanye pia, yeye ameshafungua milango”