Meneja Habari wa Kampuni ya Executive Solutions Mike Mukunza ambao ndio waandaji wa semina fupi kwa waandishi wa habari inayohusu uzinduzi wa kampeni ya Tanzania Breweries itakayojulukana kama ‘100% Tanzanian Flava’ yenye lengo la kuwaunganisha Watanzania nchini kote.


Pichani Juu na Chini ni Meneja wa Bia ya Kilamanjaro Lager George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina fupi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) inayohusu uzinduzi wa kampeni mpya ya bia hiyo itakayogharimu Shilingi Bilioni 2.3 za Kitanzania kwa kipindi cha muda wa miezi sita.Mwandishi wa Habari kutoka TBC Angela Msangi akitoa maoni yake kuhusiana na Kampeni hiyo wakati wa semina ikiendelea.


Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions Bw. Aggrey Marealle akitoa shukrani kwa waandishi wa habari kwa ushirikiano wanaoutoa kwa kampuni ya Tanzania Breweries.


Kampuni ya Bia ya Tanzania TBL kwa kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Larger leo inazindua kampeni itakayojulukana kama ‘100% Tanzanian Flava’ itakayoendeshwa kwa muda wa miezi sita .

Akitoa ufafanuzi juu ya kampeni hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe amesema kampeni hiyo imesheheni mambo mbali mbali mazuri na yenye kutuunganisha watanzania na kutufanya tuongee lugha moja.

Amesema kampeni hii itaanza kwa kuzindua stemp ya 100% Tanzanian Flava ambayo ndio itakuwa kama chombo cha mawasiliano wakati wa kampeni hii, ambayo imetengenezwa ili kumpa mteja raha lakini pia lazima iache ujumbe.

Ametaja ujumbe huo kuwa ni ‘Sherehekea Kilicho Chetu’ (Celebrate what is ours).

Bw. Kavishe amesema mambo mbalimbali yatakayokuwa yakifanyika wakati wa kampeni hiyo ni kuwaonyesha wateja jinsi gani wanawapenda na kuwajali.

Uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo unafanyika leo jioni katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.

source:MOblog