PHILLIP PHILLIPS

Philip Philips(Pichani) akitokwa na machozi usiku wa jana tarehe 23 baada ya kutangazwa mshindi wa American Idol 2012.

Kijana Phillip Phillips jana ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa American Idol kwa rekodi ya kura za watazamaji milioni 132.

Ikiwa ni msimu wa 11 tangu shindano hilo la kutafuta mwanamuziki mwenye kipaji nchini Marekani lianzishwe, limekuwa ni miongoni mwa show zinazotazamwa zaidi katika TV nchini Marekani.

Philip mwenye umri wa miaka 21 kutoka Mji wa Georgia, kusini-mashariki mwa US. Aliwashukuru wapiga kura kwa kumfikisha hapo kabla Mtangazaji Ryan Seacrest hajamtaja kuwa mshindi.

Jessica Sanchez (16) kutoka California alichukua nafasi ya pili baada ya kutokufanya vizuri sana katika onyesho la fainali kabla kura hazijapigwa.

J-LO, Rihanna ni miongoni mwa wanamuziki waliotumbuiza fainali hiyo ya kihistoria.

PHILLIP PHILLIPS