Airtel wamezindua gharama mpya kwa watumiaji wa Blackberry ambapo sasa unaweza kujiunga na kifurushi cha wiki nzima kwa shilingi elfu tano tu. Hii inamaanisha Airtel sasa wanakuwa ndio wanakuwa na gharama nafuu zaidi za Blackberry Internet Service (BIS) ambapo kabla tIGO na Vodacom ndio walikuwa na huduma ya Internet ya wiki kwa shilingi 7,000 huku zantel ya kwao ikiwa shilingi 11,000. Kujiunga unatakiwa kutuma neno KAMILI7 kwenda namba 15344 na utaunganishwa.
Kitu pekee ninachokitegemea hapa ni kuongezeka kwa wateja watakaohamia Airtel na kama hawajajipanga wataishia kuwa kama tIGO ambao ukiwa Dar es Salaam kuna baadhi ya maeneo BIS ina kasi ndogo mno inazidiwa hata na mtu anaetumia WAP. Mfano ni ukiwa Kinondoni na Mwenge ambako nadhani kuna wingi wa watu.
Zaidi ya hapo tunawashukuru kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha watumiaji wa Internet kwa kupunguza bei ya BIS

source:tanganyikan blog