Wanafunzi wa Mbagala kuu Primary School wakiwa na zawadi zao kutoka Whitedent.


Nawapongeza Whitedent kwa hili kwa sababu ya zoezi lao kubwa lakini lenye urahisi wa kupata zawadi ambalo wamekua wakiliendesha kupitia TV, T he Whitedent manufacturers Chemi & Cotex Industries Ltd jana wametoa zawadi mbalimbali yakiwemo matank ya maji kwa shule mbili za primary Dar es salaam..

Alfur-Qaan Primary School iliyopo Ilala Malapa Mferejini na Mbagala Kuu Primary School wilayani Temeke ambapo kila shule imepata tank lenye kuhifadhi maji kwa lita elfu tatu, mara ya mwisho kwa Whitedent kufanya Quiz kama hii ni 2008, Mwaka huu imerudi tena na itafanyika kwenye mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.

Ili kupata washiriki wengi zaidi, inaendeshwa campaign ya wiki nzima kupitia TV ambapo mtangazaji atakua anauliza swali kuhusu shule na wanafunzi watakua wanatuma msg kujibu ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi ambapo wanafunzi wanaweza kuiwezesha shule yao kushinda tank la maji kupitia maswali yanayoulizwa kwenye TV kila alhamisi saa moja kamili mpaka na nusu usiku na kurudiwa jumapili saa sita kamili mpaka na nusu mchana, imeanza may 17 2012 inaisha July 12 2012.

Michael Omari akiwa na zawadi ya Polytank.

Source:millardayo.com