KIM POULSEN


Kim Poulsen ametaja kikosi cha Taifa Stars ambacho leo (Juni 2 mwaka huu) kitakuwa uwanjani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.

Amefanya mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu kilicheza mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.

Amir Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia mazoezini siku moja kabla ya safari.

Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;

Kipa; Juma Kaseja

Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani

Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto

Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa

Wachezaji wa akiba; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.

Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).

Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.

Mwamuzi; Slim Jedidi (Tunisia)

Mwamuzi msaidizi namba 1; Bechir Hassani (Tunisia)

Mwamuzi msaidizi namba mbili; Sherif Hassan (Misri)

Mwamuzi wa akiba; Youssef Essrayri (Tunisia)

Mtathmini wa waamuzi; Rachid Medjiba (Algeria)

Kamishna wa mchezo; Saleh Issa Mahamat (Chad)

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MOblog