Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Balozi amesemaIsrael itatuma timu ya Wataalamu kuja kufanya utafiti wa Ugonjwa wa Moyo ambao umekuwa ukiwashambulia watoto hasa kutoka maeneo ya Pemba na kutafuta njia nzuri za kuweza kukabiliana na tatizohilo.

Balozi Idd ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Abeid Aman Karume kutoka ziara yake ambapo alizitembelea Nchi zaIsrael,Cubana Ras El kheima.

Amesema kuwaIsrael imepata mshangao mkubwa kwa kuona kuwa watoto wadogo wengi kutokaZanzibarwanakabiliwa na matatizo hayo ya ugonjwa wa moyo jambo ambalo si la kawaida kwa hivyo wameona iko haja ya kujaZanzibarkufanya utafiti juu ya maradhi hayo.

Balozi Seif amesema kuwa mbali ya maradhi hayoIsrael imeahidi kutoa nafasi za mafunzo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwani wao wanachuo maalum cha kufundishia sualahilokutokana na nchiyaokuwa ni jangwa kwa hivyo wanautaalamu wa kutosha.

Akizungumzia juu ya sula la kilimo cha ufugaji wa Samaki amesema kuwa Isarael pia ipo tayari kusaidia Zanzibar kwa wananchi walioanzisha ufugaji wa Samaki na zaidi kisiwaniPembaili waweze kufanya shughuli hiyo kwa utaalamu zaidi na kujipatia kipato zaidi.

Kuhusu suala la maafa Balozi Seif amesema kuwaIsrael ipo tayari kuisadiaZanzibarkwa kuipatia vifaa na mbinu za kuweza kujikinga na maafa na pia kuwasomesha wananchi waZanzibarkuhusu masuala hayo na tayari nafasi mbili kwa watu waZanzibarwamepatiwa kwenda nchi hiyo mwezi ujao

Kwa upande wa Cuba Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa nchi hiyo imekubali kuongeza madaktari Zanzibar wa maradhi mbalimbali na pia kutoa madaktari watakaoweza kuwafundisha wanafunzi wanaosomea fani hiyo Zanzibar.

Aidha Balozi Seif amesema mbali na kuleta madaktari pia patakuwa na nafasi kwa nchi hizo mbili kubadilishana uzoefu katika fani hiyo kwa kutembeleana.

Mbali na shuguli hizo Makamu wa Pili wa Rais waZanzibaralifanyiwa matibabu ya Macho nchini humo ambapo hali yake ipo nzuri na yakuridhisha.

Huko Ras El Kheima alisema kuwa nchi hiyo imeendelea katika ufugaji wa Lulu ambapoZanzibarinaweza kufaidika katika sokohilokwa wataalamu kutoka nchi hiyo kujaZanzibarkuweza kuwafundisha wananchi ili na wao waweze kutoa zaohilokwa wingi na soko kuu kuwa huko.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd aliondoka Zanzibar May 5,2012 kwa kuanzia ziara yake nchini Israel,Cuba na hatimaye Ras El Khaeima na kurejea Zanzibar June 2,2012.

source:MOblog