Wilfred akipeperusha bendera ya Tanzania kwa furaha baada ya kuifikisha katika kilele cha mlima mrefu kuliko yote duniani, mlima Evarist (picha ya mtandaoni)

Nchi yangu ya Tanzania haijawahi kuishiwa vituko kwa hakika. Wakati wanasiasa wanaofuja mali za umma wakiwa wanapokewa kwa maandamano kama mashujaa katika majimbo yao, Watanzania ambao wanaliandikia taifa hili historia za kipekee katika nyuso za dunia, wanaendelea kuonekana hawana maana huku wakienziwa kwa mambo yenye kustaajabisha hata kuyasikia. Unajiuliza inakuwaje? Sikia hii

Wakati baadhi ya wabunge waliovuliwa uwaziri kwa tuhuma za kulisababishia taifa hasara kubwa wakipokelewa kwa shangwe na nderemo katika majimbo yao waliporejea huko hivi karibuni, Mtanzania wa kwanza katika historia ya dunia, kuwahi kupanda mlima mrefu kuliko yote duniani, mlima wa Evarest, ndugu Wilfred Moshi, amerejea nchini na kupokelewa kama mtu wa kawaida sana kana kwamba hakuna cha maana alichokifanya kwa ushujaa wake huo.

Na kana kwamba hiyo haitoshi, kitendo ambacho binafsi nakiona ni cha dharau ya hali ya juu mno, kikajiri pale alipopokelewa na viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro waliokuwa katika maadhimisho sijui ya siku ya maziwa, ambao eti wakaishia kumzawadia maziwa…..

Tizama Video ifuatayo kusikia mkasa mzima, kama ambavyo umeripotiwa na kituo cha UTV kupitia taarifa yao ya habari ya saa mbili usiku wa leo
Maziwa? Kwa kuliandikia taifa historia? Ama kweli, taifa langu nilipendalo lina watu ambao hatujitambui. Ningali najiuliza tena…zawadi ya maziwa? Kwa kuifikisha bendera ya Tanzania katika kilele cha mlima Evarest? Hakika ninakaukiwa na maneno muafaka kwakweli….

source:jukwahuru