MENEJA wa Bendi ya Coast Modern Taarab ya Jijini Dar es Salaam Yahya Limwange amwetaka wasanii wa muziki huo kukaa chini na kutunga mashairi yanayokubalika katika jamii .
Limwange amekerwa na baadhi ya wasanii kuvamia tasnia hiyo ya muziki kwa madhumuni ya kusaka pesa na kuacha maadili halisi ya muziki wa taarab hivyo kujikuta wakitunga albamu utitiri zisizo kuwa na maana. Meneja huyo wa Coast Modern Taarab amesema utoaji wa albamu utitiri ndani ya muda mfupi ni hatari kabisa na ni kuukosea Heshima muziki huo.

Alianza kwa kuzungumzia utungaji wa albamu mpya kuwa imejawa na nyimbo kama Dua la Kuku na Mpende akupendaye. Na kadhalika

Coast Modern Taarab usiku wa kuamkia leo walikuwa katika ukumbi wa Mkpa Jijii Mbeya wakisindikiza usiku wa kumpata ni Miss Redd’s Mbeya . Bendi hiyo imetua jiji hapa mapema juzi asubuhi na kina Nuru Njama, Wastara MC, Rehema Salum, Maua Tego, Kibibi Yahya Mpiga gitaa la bass Adam Kilinda, Mpiga Gitaa Solo Matole Hussein na Mpiga Kinanda Yusuph Tego.