Mkurugenzi wa Michezo Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Ndugu Phares Magesa
Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani, Danna Banks
Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro Hasheem Thabeet ,Viongozi wa TBF, Makocha, Wachezaji wadau wote wa michezo.

Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru TBF kwa kazi kubwa walioifanya ya kuakikisha mafunzo haya yanafanyika katika kiwango kizuri , zaidi napenda kuwashukuru Coca cola kupitia kinywaji cha Sprite kwa kuendelea kufadhili mchezo wa Mpira wa kikapu hasa katika ngazi ya Vijana wadogo, pia nawashukru sana watu wa Marekani kupitia Ubalozi wao hapa Dar Es Salaam kwa kusaidia kuendeleza vijana wetu kupitia mchezo wa kikapu.

Kipekee na penda kumpongeza Hasheem Thabeet kwa kuonyesha thamani yake katika mchezo wa Mpira wa Kikapu na kukubali kutumia muda wake kwa ajili ya Vijana wadogo kuwapa mafunzo na kuinua ari kwa vijana wetu ili nao wapate kuwa na ndoto na kufika pale alipo yeye. Ni matumaini yangu mafunzo haya mmeyapokea vizuri mtayazingatia na mtakapo rudi kwenye shule zenu nanyi mkawe mabalozi wazuri na walimu kwa wenzenu ambao hawakupata nafasi kama hii mliyoipata Mikoa iliyoshiriki kliniki hii ya mwaka huu ni Mwanza, Tanga, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa Dar es Saalaam hivyo basi ni matumaini yangu mwakani mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani itashiriki, naomba wafadhili wajitokeze zaidi kuunga mkono jitihada za Cocacola na Hasheem Thabeet ili tuibue vipaji vingi zaidi katika kikapu.

Ndugu zangu serikali ipo pamoja nanyi katika michezo kama mnavyofahamu wote kuwa mashindano ya Umiseta na umitashumta yamerudishwa rasmi mashuleni, hivyo mafunzo haya waliyopata vijana hawa basi yatasaidia kuwaimarisha kimbinu za kimchezo na ni matumaini yangu mikoa iliyoshiriki hapa itafanya vizuri kwenye mashindano yajayo ya shule za sekondari na msingi.

Serikali itaendelea kushirikiana na vyma vya michezo vyote nchini katika kuhakiksha michezo inaimarika mashuleni ikiwa ni pamoja kupeleka walimu wengi zaidi wakasomee taaluma hii katika vyuo vyetu mbali mbali, ikiwa ni sambamba na kuongeza uwezo wa vyuo vyetu vya ualimu kufundisha michezo.

Narudia tena wito wangu kuwa michezo ni sehemu muhimu ya kujenga vijana wetu kiafya, kielimu na kimaadili na hata kiuchumi hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu, wanamichezo, wazazi, walezi na wakuu wa shule zote nchini kuhakisha vijana wanapatiwa fursa ya kushiriki katika michezo.

Nafahamu kuwa changamoto ya miundombinu ya michezo bado ni tatizo kubwa katika nchi yetu, hivyo basi Serikali itafanya kila jitihada kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha tatizo hili linashugulikiwa ipasavyo katika ngazi zote.

Maombi yenu kwa serikali ya kuomba mpewe kipaumbele katika ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndani wenye hadhi ya kimataifa kama wezenu wa soka na riadha wanavyofaidika na uwanja mkuu wa Taifa, nimeyachukua na nitayafikisha katika ngazi husika ili yaweze kushugulikiwa.

Nawashukuru sana wadhamini wa mafunzo haya kampuni ya Cocacola kupita SPRITE na Hasheem Thabeet na nitoe wito kwa wanamichezo wengine Tanzania kuiga mfano wa Hasheem Thabeet wa kurudisha fadhila kwa jamii nzima ya watanzania na nia yake njema ya kuona vipaji vingine vinaibuka Tanzania.
Niwatakie heri katika mafunzo mengine kama haya yatakyofanyika Arusha juma lijalo.

Natoa wito tena kwa makampuni mengine yajitokeze kudhamini michezo na hususani mchezo wa kikapu.

Niwatakie Safari njema wale wote watakaosafiri kurudi mikoani na niwashukuru wote kuanzia Walimu wenu,Wazazi kwa kuwapa ushirikiano mzuri katika kuchangia kufanikisha malengo yenu.

Asanteni kwa kunisikiliza na sasa nimeyafunga rasmi mafunzo haya ya SPRITE HASHEEM THABEET CLINIC 2012.

source:aizmelaleo