May na June imekuwa miezi yenye habari njema kwa kundi la Hip Hop la nchini Kenya, Campmulla. Mwezi uliopita kundi hilo lilitajwa kuwania tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act Africa, na sasa vijana hao watano wamekamata deal nono kutoka kwa Universal Music Group. Mkataba huo uliosainiwa nchini Afrika Kusini unawafanya wawe label moja na P-Square wa Nigeria ambao nao walisaini mkataba huo wiki hii. Nao pia kama Peter na Paul Okoye, wamejiunga na label iliyo na wasanii zaidi ya 100 duniani. Miongoni mwa wasanii wakubwa waliochini ama waliowahi kuwa chini ya UMG ni pamoja na Young Jeezy, Wale, William, Tyga, Soulja Boy, Shania Twaim, Shantele, Steve Wonder, Akon, Rick Ross na Rihanna. Wengine ni Nicki Minaj, Ne-yo, Nas, Melanie Fiona, Madonna, Lil Wayne, Keri Hilson, Kanye West, Justine Bieber, Jennifer Lopez, Drake, Dr. Dre na wengine wengi. Makao makuu ya UMG yapo Santa Monica, California nchini Marekani lakini ina matawi yake sehemu mbalimbali duniani kote.

source:BongoFlavortz