CHIDI BENZMfalme wa Ilala Rapper Chidi Benz Chuma baada ya kuachia single yake mpya ambayo ni kolabo na mwimbaji Taarab Khadija Kopa, ameahidi kutoa single yake nyingine mpya ambayo ni kama bonus inayohusu yeye kuomba msamaha kwa yeyote aliemkosea.

Ameomba msamaha kutokana na ukorofi wake aliowahi kuufanya, kutokueleweka, mikwaruzano na kutokujua kudil na mashabiki wake vizuri.

Chidi amesema amebadilika na kuna vitu vingi ambavyo alivifanya muda uliopita na sasa ameamua hatovifanya tena kwenye maisha yake yanayoendelea, hatorekodi nyimbo tena kiholelaholela, atahakikisha haitokei tena kutoa nyimbo zikasambazwa bila uhakika na pia ataacha kufanya matukio ambayo hayaendani na kazi bora.

source:millardayo.com