BONDIA Alen Kamote wa Tanga anatarajiwa kuzichapa na Deo Njiku wa Morogoro katika pambano la raundi 10, la uzani wa kg 61kuwania ubingwa wa IBF Afrika litakalofanyika Septemba 19, kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mratibu wa Pambano hilo, Promota Abbas Mwazoa alimweleza mwandishi wa habari hizi jana kuwa maandalizi ya pambano hilo yanaendelea vizuri .

Alisema pambano hilo litatanguliwa na  mapambano ya utangulizi kati ya Haji Juma atazichapa na JJ Ngotiko katika pambano la raundi 8, uzito wa kg 55.

Rajabu Mahoja atapanda uliongoni kuzichapa na Jumanne Mohamed katika pambao la raundi 8 lenye uzito wa kg 57, wakati bondia Saidi Mundi ataonyeshana ubabe na Khamis Mwakinyo kwenye pambalo la raundi 6 kwa uzito wa kg 59.

Pia, bondia Zuberi Kitandula ataamva Ibrahimu Habibu kwenye pambano la raundi 6 lenye uzito wa kg 53 wakati Abdallah Mapoka a atazichapa na Selemani Hamza pambano ambalo litakuwa la raundi 4 lenye uzito wa kg 55.

Mohamed Kidari atapanda ulingoni kuzichapa na Mohamed Ameme katika pambano la utangulizila  la raundi 4 lenye uzito wa kg 63 huku Puguto Omari akitarajiwa kuzichapa na Patric Kimweri pambano la raundi 4 lenye uzito wa kg 48.

Naye Mashaka Spoiler  atazichapa na Mohamed Sudi katika pambano la raundi 4 lenye uzito wa kg 66 huku bondia Athumani Boxer na Lucas Michael wakihitimisha mapambano hayo kwa kucheza pambano la raundi 4 lenye uzito wa kg 61.

source: