Diamond Platnums.


Mwimbaji staa wa Tanzania Diamond Platnums ambae alitangaza kwamba mwaka huu utakua wa kolabo atakazofanya za wasanii wengine, amesema huo mpango unakaribia kufikia mwisho.

“sikuwahi kufanya kolabo sana mwanzoni kwa sababu nilitaka kuonyesha watu uwezo wangu kwanza, baada ya hapo ndio nikaamua kufanya kolabo ambazo sasa naelekea kuzisitisha na nyingine nimefanya mpaka na wasanii wa nje ya Tanzania, mpaka sasa zimefika nane na nilitaka kumi tu na ninafikiria hizo mbili zilizobaki nifanye zangu tu” – Diamond Platnums.

Kuhusu ishu ya kumchaji msanii anaehitaji kolabo nae, Diamond amesema “kiukweli inategemea uhusiano wangu na wewe lakini kama hatujuani, kama umekuja kibiashara kwa sababu muziki ni biashara utalazimika kunilipa milioni tano kama ni verse na Chorus itakua milioni kumi nafanya na Video pia, muziki umebadilika sasa hivi kwa sababu kwenye show watu wanakula milioni 5, 7 mpaka kumi”

Mpaka sasa Diamond amesema hajawahi kumchaji msanii yeyote pesa kwa ajili ya kolabo lakini hicho ndio kiwango alichojiwekewa yakitokea mazingira kama hayo.

sOURCE:Millardayo.com