Masanja Mkandamizaji


Tangu alipojiunga twitter Mei 14 mwaka huu Masanja Mkandamizaji au masanjawani ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi wanaomfuata. Kama ilivyo mtaani ambapo hana maringo na ni mtu wa watu hata twitter imekuwa hivyo. Lakini wapo mastaa kibao ambao mtaani wako poa lakini kwenye social media hawajabamba kwa muda mfupi kama Masanja, ni kwa nini?

Kitu cha kwanza kinachomtofautisha na waigizaji wengine waliopo twitter, masanja ameendelea kuwa yeye. Hajajaribu kuiga uhusika wa mastaa wa nje kama ilivyo kwa baadhi ya ndugu zetu ambao wanaleta Umarekani mwingi kwenye tweets zao. Jamaa ukitembelea timeline yake lazima ufurahi, ni utani na vichekesho kwa kwenda mbele huku akigusa kila kona na bila kumuogopa mtu. Pia amekuwa mstari wa mbele kwenye kutengeneza Trending Topics ambazo mara nyingi watu huzidakia na kuendelea kuzitumia katika tweets na mwisho wa siku ni raha kuzisoma tweet za TT husika.

Tofauti na watu maarufu wengine ambao akiingia twitter anafanya kufuata watu wachache anaowafahamu, Masanja yeye anafuata asilimia kubwa ya Watanzania. Mara ya mwisho nilipoangalia idadi yake ya followers alikuwa na followers 2,288 na yeye anafuata 2,133. Ukipiga hesabu ya haraka ni anafuata 98% ya followers kitu ambacho ni mara chache kuiona kwa wenye majina wengine.

Ugonjwa mwingine wa wenye majina bongo ambao Masanja kafanikiwa kuuepuka ni ile tabia ya kupotezea tweets za watu wanaomsemesha. Pamoja na kuandikiwa na watu wengi sana lakini jamaa anajibu kila mtu anaemuuliza swali au kumsemesha, anashukuru pale mtu anapomsifia na mwisho ni ile tabia ya kujichanganya kwenye mazungumzo ya wafuasi wake. Unajua watu wengi wanachukulia ukiwa maarufu wewe ndiye unatakiwa kusemeshwa au ukiongea wewe ndio unajibiwa na unaamua kujibu au kutojibu, Na asilimia kubwa ukimuandikia kitu au kumsifia badala ya kusema asante anaishia ku-Retweet. Kwa Mwanawani yeye kukiwa na kitu kinachofurahisha atakujibu au ku-Retweet na kuongeza utani wake.

Naamini akiendelea kuwa kama alivyo ndani ya muda mfupi ataingia kwenye orodha ya watu wenye followers wengi Tanzania na pia wenye ushawishi kwenye social media zaidi ya wanasiasa wengi ambao wamejiunga muda mrefu tu.

source:tanganyikan