Abiria mwingine wa basi amefariki dunia mara tu alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hivyo kufikisha idadi ya watu 10 ambapo wanaume ni 7 na wanawake 3. Gari la Abiria aina ya Coaster T188 AWE lililokuwa likitokea Mbeya Mjini kuelekea Kyela liliparamiwa na Lori aina ya Fuso T 658 ASN lililokuwa likitokea nchini Malawi, kufuatia mfumo wa breki za Lori hilo kushindwa kufanya kazi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Lori hilo lilikuwa likitokea njia ya Malawi kuja mjini Mbeya lilianza kuyumbayumba na kushindwa na wakati huo huo basi la Abiria lilikuwa likipandisha kwenda Kyela. Dereva wa basi la Abiria amefariki dunia papo hapo huku Kondakta wake akijeruhiwa. Majeruhi wamekimbizwa Hospitali ya Rufaa huku wawili hali zao zikiwa mbaya.

Maafisa wa Jeshi la Polisi wamethibitisha kutokea kwatukio hilo la kutisha

sourcejaizmelaleo.blogspot