Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Paul Chizi na amewasimamisha kazi wakurugenzi wanne kutokana na “ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, ambao umetishia uhai wa shirika hilo muhimu kwa taifa.”

Kutokana na hatua hiyo, Dk Mwakyembe amemteua rubani wa siku nyingi katika shirika hilo, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Chizi.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Omary Chambo alisema Dar es Salaam jana kwamba Waziri amefikia uamuzi huo kutokana na taratibu za uteuzi kwa wafanyakazi wa umma kutokufuatwa.

Alisema nafasi aliyopewa Chizi haikutangazwa kama sheria na kanuni zinavyotaka… “Uteuzi wake haukufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, hivyo kupitia Sheria Na 8 ya mwaka 2002 na kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2003 Na 17(4), Dk Mwakyembe ametengua uteuzi huo kuanzia jumanne.”

“Kanuni hii inaeleza bayana kuwa kama mtumishi atakuwa ameteuliwa kwa…

View original post 246 more words