2012 anaingiza euro milioni 29.2 Milioni (paundi 24.3m)
2011 alikuwa anaingiza euro milioni 27.5
Anautajiri wakiasi cha dola milioni 160
Club aliyopo sasa Real Madrid
Ni nyota wa timu ya Real Madrid ambaye amekuwa hapo kwa misimu mitatu sasa na aliweza kufunga magoli mengi kwenye ligi ya La Liga kwa kufunga magoli 32 katika mechi 26 kwa msimu uliopita. Anatumia mitandao ya kijamii akiwa na fans milioni 26 mara tatu ya wachezaji wengine kwenye mtandao huo na anafollower milion 3 ambayo ni moja ya kivutio kwa wadhamini kama vile Nike, Armani, coca-cola and Castrol.

Mchezaji staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameweka wazi kwamba anatamani aendelee kuichezea club hiyo kwenye maisha yake yote ya soka yaliyobaki.

Gazeti ya Uingereza (The Sun) limeandika kwamba Ronaldo amesema kama ingekua ni uwezo wake angesaini hata mkataba wa miaka kumi wa kuichezea club hiyo ila hilo linashindikana kwa sababu kuna taratibu zilizowekwa na club.

Ronaldo ambae anajiandaa na Euro 2012 mpaka sasa ameshaifungia Real Madrid magoli 112 toka ajiunge nayo mwaka 2009 ambapo inakua club ya kwanza yeye kuifungia magoli mengi toka aanze soka, aliifungia Manchester United magoli 84 wakati alipoichezea kuanzia 2003-2009.

source:millardayo.com