WAKATI zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu za kuwania uongozi katika klabu ya Yanga likimalizika leo, kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo imewaita wanawake wenye sifa na vigezo kujitosa kuwania uongozi.

Wito huo umetolewa na katibu wa kamati hiyo, Francis Kaswahili alipokuwa akizuzungumzia zoezi la uchukuaji fomu na kusema kwamba anasikitishwa na jinsia hiyo kutojitokeza mpaka sasa.

“Kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana, yaani Yanga ni klabu kubwa na yenye wanachama wa kila rika lakini nashangazwa mpaka sasa hakuna jinsia ya kike iliyojitokeza kuchukua fomu…jamani waandishi wahamasisheni kina mama wajitokeze,”alisema.

Aidha, Kaswahili aliongeza kuwa mpaka sasa wagombea 19 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi utakaofanyika Julai 15.

WADAU maarufu wa michezo nchini, Muzamil Katunzi na Yono Kevela ni miongoni mwa wanachama wa klabu ya Yanga ambao wamejitosa kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Julai 17. na kwamba hadi hivi sasa ni wagombea 19 wamechukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika klabu ya Yanga yenye makzi yake Mtaa wa Jangwani Jijini Dar es Salaam.