Kocha mpya wa timu ya kandanda ya Villarreal ya Uhispania, Manuel Preciado, amefariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo hii leo, akiwa na umri wa miaka 54.


Preciado aliyekubali wadhifa wake hapo jana, alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo, iliyoshuka daraja kutoka ligi kuu ya Uhispania msimu uliopita. Mtandao wa Villarreal umearifu kuwa timu nzima imetuma rambirambi zake kwa familia ya kocha huyo. Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Uhispania, Vicente del Bosque, amesema wameshtushwa na kifo cha Preciado, akiwa nchini Poland na timu yake wakijiandaa kwa michuano ya kombe la Ulaya, UEFA EURO 2012. Preciado alizichezea timu kadhaa, ikiwemo Racing Santander, na aliwahi kuwa kocha wa Racing, Levante, Murcia na Sporting Gijon.