Waajiri wa Wafanyakazi wa ndani mkoani Mbeya wametakiwa kuwajali wafanyakazi hao kwa kuwapatia elimu ili waweze kumudu maisha.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Redio Mbeya FM katika kipindi cha TABARADI jioni ya leo Mkurugenzi Mtendaji Mahmoud Komba wa Kampuni la MOD Intergrated Solution and Awereness amesema elimu ni kitu cha muhimu sana kwa kundi hili lakini kutokana na unyama unaofanywa na waajiri wao wamejikuta katika hali ngumu zaidi. Pia Komba ameongeza kusema Ujasiriamali nis uala ambalo nchini Tanzania linatakiwa kupewa kipaumbele ili kuweza kukidhi mahitaji ya kila siku. Katika suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema watanzania hususani walioko Mkoani Mbeya kuchangamkia masomo ya ujasiriamali ili kuweza kubana mianya ambayo ingeweza kuwakosesha fursa muhimu. Ameongeza kusema uwanja wa ndege wa Songwe unaomalizikia kujengwa utaleta watu kutoka mataifa mbalimbali ambao watakuwa wakija kufanya biashara na wakazi wa Jiji la Mbeya lakini ili weze kuonekana inalipa ni muhimu kujikita katika ujasiriamali.

UJASIRIAMALI ni ile hali ya kubuni jambo fulani au kutatua tatizo lilopo katika jamii kwa kutengeneza njia au zana au kifaa na kuziingiza katika soko

source:aizmelaleo