Hii movie ilikua ni dili waliyoipata waigizaji watanzania wawili tu Monalisa na Marehemu Steven Kanumba na walitakiwa kwenda kuiigiza Ghana kuanzia May mwaka huu lakini mpaka sasa bado haijulikani ni nini kilichosababisha Monalisa asiitwe kwenda kuanza kazi.
Monalisa amesema mpaka sasa hivi hawezi kuiongelea sana kwa sababu hajui kinachoendelea na hajawasiliana na hao watu toka January lakini anachofahamu ni kwamba movie ilitakiwa kuanza kuchezwa May mwaka huu.
Amesema “Producer na Director wa hiyo movie alikua mjamzito kwa hiyo alirudi Marekani mpaka ajifungue ndio arudi Ghana kwa ajili ya kushoot, sasa sijajua lini itaanza kufanyiwa shooting manake sijawasiliana nao kwa muda mrefu”
Mona amesema Waandaaji wa hiyo movie walipata taarifa za kifo cha Kanumba na hawajazungumza chochote kuhusu kumchukua mtu mwingine wa kuziba nafasi yake kwenye hiyo movie iliyotakiwa kuchezwa Ghana, Egypt, Russia na Dubai.
Mwenye movie ni Yaboa Annie Mghana ambae anaishi na kufanya kazi Marekani huko Hollywood ambapo kama unakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu Marehemu Kanumba na Monalisa walisafiri kwenda Ghana kwa ajili ya kutengeneza Trailer ambayo ilipelekwa Hollywood ili iombewe pesa ya kutengenezwa ambapo sasa ndio wangerudi kwa ajili ya kuanza kuicheza.
(Picha zote hizi zilipigwa na Camera ya Marehemu Kanumba walipokwenda Ghana ambapo aliziweka kwenye blog yake, R.I.P)

sources:millardayo