Mkazi Rozi Mwadala (60) wa Kijiji cha Malamba, wilayani Mbarali Mkoani Mbeya amezikwa akiwa haki Juni 2 mwaka huu baada ya kutuhumiwa kujihusisha na imani za ushirikina.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alihisiwa kuwa ni mshirikina kutokana na matukio yaliyopo kijijini hapo licha ya kwamba kuweza kugundua ni kazi ngumu sana.
Mjomba wa Marehemu Wilson Legembo alishuhudia marehemu akizikwa hai na kaburi lake likifukiwa na kuongeza kwamba muda mfupi baada ya kuzikwa aliitwa mganga wa jadi kwa ajili ya kupiga ramli.

Ramli ilipopigwa mganga huyo wa jadi akasema marehemu ndiye aliyehusika na kifo cha mkazi mwingine wa kijiji hicho marehemu Frank Lingo(25),aliyefariki Juni Mosi mwaka huu kwa maumivu kwenye sikio na jicho.

Viongozi wa Muungano wa Jamii Tanzania(MJATA) wakiongozwa na Chifu Soja Masoko walifika eneo la tukio siku moja baada ya tukio la mtu kuzikwa akiwa hai Bi. Rozina,kitendo ambacho walikilaana vikali na kuwataka Waganga wa jadi kutoleta uchonganishi unaopelekea watu wengi kuuwawa pasipo hatia.

Mchungaji wa Kanisa la Baptist John Laus alifika kwenye msiba kushuhudia tukio hilo la kikatili la mtu kuzikwa akiwa hai,ambapo aliwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linaendelea na uchunguzi.

sources:jaizmelaleo