Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Mwalimu J.K.Nyerere iliyopo wilayani Momba katika mji mdogo waTunduma aliyejulikana kwa jina la Boazi Essau Mwalusanya amejinyonga hadi kufa.

Sababu za kujinyonga kwake hazijajulikana mpaka sasa. kabla ya kujinyonga mwanafunzi huyo alikuwa akiongea lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiarabu na alikaririwa akisema atakufa mwezi wa sita na kudai kuwa atakumbukwa kama msanii maarufu aliyekufa hivi karibuni kwa mtikisiko wa ubongo. Mwanafunzi huyo aliyekuwa mshiriki wa mafunzo ya skauti amezikwa Juni 6 mwaka katika makaburi ya Migimbani mjini Tunduma.

Maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya wamethibitisha tukio hilo.

sources:jaizmelaleo