PAMOJA na Waziri wa Maendeleo ya mifugo na uvuvi,Dk. David Mathayo kupiga marufuku uingizaji wa mifugo wilayani Moshi Vijijini, kutoka Kenya, mifugo hiyo inaendelea kuingia kama kawaida.
Wiki iliyopita kupitia mkutano na waandishi wa habari, Dk Mathayo alipiga marufuku uingizaji holela wa mifugo kupitia njia za panya zilizopo katika Kijiji cha Lotima wilayani humo. Waziri Mathayo alisema ni jambo la hatari, kuruhusu mifugo kuingia nchini bila kibali na wala kuchunguzwa na maofisa mifugoili kujua kama ina magonjwa ama la.Dk. Mathayo, alisema mifugo yote inayoingia nchini, lazima ipate kibali cha Serikali na ipitie katika njia rasmi. Hata hivyo uchunguzi wa kina uliofanywa,umebaini kuwa makundi ya ng’ombe kutoka Kenya yanaingizwa katika Wilaya ya Moshi Vijijini na kupelekwa katika mnada wa Njipanda ya Himo. Uchunguzi huo umebaini kuwa Juni 5 mwaka huu ng’ombe 200 waliingia wilayani humo, kupitia katika Kijiji cha Lotima wakitokea Kenya na Juni 29 kundi lingine la ng’ombe 56 waliingia nchini bila kibali.

Vyanzo vya habari vimedokeza kuwa uvushaji huo wa ng’ombe hao, umekuwa ukifanywa na wafanyabiashara kutoka Kenya wakisaidiwa na baadhi ya askari mgambo na viongozi. Baadhi ya wafanyabiashara wamelalamikia usumbufu mkubwa wanaoupata kutoka kwa baadhi ya viongozi hao wanaodai rushwa ya hadi Sh2 milioni, hata kama wafanyabiashara hao wana vibali halali.

Mtendaji wa Kijiji cha Lotima,Kassim Mongi ,alipohojiwa kuhusu tuhuma hizo, alikanusha na kusisitiza kuwa tatizo la uingizaji wa mifugo limedhibitiwa

SOURCE:Jaizmelaleo