Marehemu Bob Makani mwenye vazi jeupe.


Muasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mohammed “Bob” Makani amefariki Dunia jioni ya jana jijini Dar kwenye hospital ya Aghakhan ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA amethibitisha hilo kwa njia ya simu kutoka Kanda ya kusini walikokuwa wakifanya mikutano yao ya hadhara.

Mbowe amesema kuwa Marehemu Makani alikuwa akiugua kwa muda mrefu na kupelekwa hospitali mbalimbali kwa matibabu ikiwemo nje ya nchi na baada ya kifo chake hiyo jana Mwili wake umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa hifadhi. Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach jirani na Rainbow. (stori imeandikwa na Mroki Mroki)