George Saitoti na (kulia) Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga wakionekana katika ajali ya helikopta iliotokea leo


Imethibitishwa kuwa Waziri wa usalama wa taifa wa Kenya Profesa George Saitoti pamoja na msaidizi wake Joshua Ojode ni miongoni mwa watu saba waliofariki dunia kwenye ajali ya helicopter ya Polisi iliyotokea kati ya saa tatu au saa tano leo asubuhi huko Ngong Kenya.

Citizen Tv wameripoti kwamba inaaminika chanzo cha ajali ni kutokana na hali mbaya ya hewa ambapo helicopter hiyo ilikua na marubani wawili akiwemo mmoja wa kike.

Kifo hiki kinaingia kwenye kumbukumbu ndefu ya wakenya kwa sababu tarehe kama ya leo miaka minne iliyopita helicopter nyingine ya Polisi ilipata ajali na kuua mawaziri wawili wa Kenya.