AY na MwanaFA


Kumbe Mwana Fa na Ay waliacha kurekodi nyimbo zao kwenye studio ya B hits toka mwishoni mwa 2011? nilikua sijui.

Fa amethibitisha hilo kwa kusema ni swala la biashara tu baada ya B hits kupandisha bei zao za kurekodi.

Amesema “siwezi kusema ni bei gani lakini ni pesa ambayo unaweza kurekodi tracks kadhaa sehemu nyingine yoyote iwe Uganda au Kenya hivyo tukaona tuvute nguvu mpaka tutakapokua na uwezo na nguvu na sababu za kulipia kiasi hicho kwa studio kama B hits na tutaona kwamba kama production yao ina ubora ambao unastahili wa kulipiwa kiasi hicho cha pesa tutafanya hivyo lakini hatuna matatizo kabisa bado tunaongea na Hammy B”

Mwana FA ambae ametoa single mpya inaitwa AMEEN Ft Ay na Dully Sykes ikiwa ni zaidi ya miezi mitano kupita toka atoe single yake nyingine ya YALAITI, amesema sasa hivi kwa msanii kama yeye kulipia studio inategemea.

“inategemea kwa sababu wakati mwingine unakwenda kurekodi mahali kwa sababu unataka kuwasaidia wenye studio kwa hiyo sio fair kulipia lakini kuna wakati mwingine mi namuhitaji Marco Chali kufanya ngoma yangu, yeye anihitaji mimi kuwa producer na kutengeneza hela zake kwa hiyo inategemea lakini kama nakwenda kwa producer mkubwa nitamlipa” – Mwana FA

source:millardayo.com