Jumatatu ya leo katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknonolojia (COSTECH) kutakuwa na mjadala kuhusu mfumo wa ulinzi katika mawasiliano kama Simu, Internet na Mfumo wa malipo kwa simu za mkononi.

Kwa sasa uhalifu kupitia mawasiliano umeongezeka huku taasisi za kifedha na serikali zikilengwa zaidi na wahalifu hao, lakini hata watumiaji wa huduma za malipo ya fedha kwa kutumia simu kama M-Pesa, Tigo Pesa au Ezypesa wamejikuta wakiwa wahanga. Njia pekee ya kuzuia kitu hiki sio kuongeza ulinzi kwa sababu wahalifu nao ni wataalam na wanajua jinsi ya kuipita mifumo ya ulinzi, bali ni kutoa elimu ya namna ya kujiepusha kwa watumiaji. Kwa kutambua hilo MobileMonday ambayo hufanyika kila Jumatatu ya mwanzo wa mwezi katika ukumbi wa COSTECH jumatatu ya Juni 10 itaendesha mjadala kuhusu suala hili.

Watakaoongea ni:
Noah Maina
– Chief Network (WiA)
– Ataongelea kuhusu ulinzi katika mawasiliano ya kompyuta na kuelezea kwa kifupi kuhusu mfumo wa CERT.

Zaituni Mmari
– IT Security Specialist (IBM/Airtel)
– Ataongelea kuhusu uanzishwaji wa ulinzi katika mfumo wa mawasiliano ya kompyuta katika serikali ya Tanzania.

Edith Turuka
– Telecoms Eng (Ministry of Communication, Science and Technology)
– Ataongelea kuhusu ukusanyaji taarifa, Hatua, ulinzi katika mfumo wa LAN na namna ya sera za ulinzi katika kampuni.

Mjadala utafanyika katika ukumbi wa COSTECH na unaweza kujiandikisha kwa kubofya hapa http://momodarsecurity.eventbrite.com/

soure:tanganyikan