Baadhi ya warembo watakaoshiriki shindano la Miss Dar Inter College 2012 wakimsikiliza mwalimu wao Marlydia Boniface wakati wa mazoezi yao jana kwenye hoteli ya Grand Villa.


WAKATI shindano la kumsaka Miss Dar Intercollege 2012 likitarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) duka la vipodozi la Shear Illusions,pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi,Mustafa Hassanali wamejitosa kudhamini shindano hilo .

Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika juni 8 kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo ‘Field’.

Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alimesema kwamba Shear lenye matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihusha na uuzaji wa vipodozi halisi ‘original’ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwa warembo watakaoshiriki,huku Hassanali atatoa zawadi ya magauni ya warembo.

Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ambapo leo warembo hao ambao awali walikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada, jana walihamishia kambi yao kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Dina ameongeza kuwa mpaka sasa wameshapatikana warembo 13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na dansa aliyepata kufanya vema miaka ya nyuma, Bob Rich.

source;dewjiblog