· Fedha za safari za JK zaibwa
MAOFISA watano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa “kwa ajili ya safari za rais,” MwanaHALISI limeelezwa.
Taarifa za uhakika zilizopatikana ndani ya ikulu na wizara hiyo, zimesema kwamba maofisa hao, akiwemo Mkuu wa Itifaki, walifanikiwa kuchota Sh. 3 bilioni “kutoka benki moja nchini.”
· Bajeti kiinimacho
BAJETI ya serikali inayotangazwa kesho bungeni mjini Dodoma, imeelezwa kuwa ni “kiinimacho kingine.”
Wasomi, wanasiasa wakiwemo wabunge na baadhi ya wananchi mashuhuri wamesema, zitatajwa tarakimu tu kama ilivyokuwa mwaka jana, lakini haitakuwa bajeti ya kutekelezeka.
· Nape: Sauti ya upweke nyikani
Na Kondo Tutindaga
PROPAGANDA ni njia ya kuuza chako, kukieneza, kukithaminisha. Hapa tunajadili itikadi katika siasa. Uhai wa vyama vya siasa, pamoja na mipango thabiti na mikakati, hutegemea pia idara, ama ya propaganda au ya uenezi wa itikadi.
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa miongo mitatu ya uhai wake pamoja na miongo miwili ya vyama vya awali, kilikuwa makini sana kuteua watu wa kuongoza idara hii.
· CCM ‘imejiua’, inasubiri kuzikwa
Bila kutafuta maneno, mgogoro ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umekuzwa na kupata nguvu baada ya Jakaya Kikwete, kukubaliana na matakwa ya wachache ya kuvunja Kamati Kuu (CC) na sekretarieti yake iliyokuwa inaongozwa na Katibu mkuu wake, Yussuf Makamba. Hapo ndipo mpini ulipoanza kuungua.

Ni tukio hilo lililoingiza sektarieti na kamati kuu iliyochoka. Ikaibuka na utafiti dhaifu uliozaa falsafa ya “kujivua gamba.” Hii ndiyo dhambi ambayo inaitafuna CCM mpaka sasa; hakuna njia nyingine mbadala ya kukiokoa chama hiki.

John Kibaso, kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa zamani wa Temeke.

source:Mjengwablog