Roberto Di Matteo

Chelsea wamemuhakikishia nafasi Robert Di Matteo kwa kumchagua kuwa kocha wa timu hiyo. Tajiri wa Chelsea Abramovich, alipendezwa zaidi na jinsi Di Matteo alivyokuwa akiiendesha timu.

Abramovich aliamua wiki iliyopita kwamba anamtaka Di Matteo na jumatano usiku, uongozi ulitangaza kumpata mkataba huo Di Matteo.

Di Matteo alisema, ‘Ninashukuru kuteuliwa Mkurugenzi na kocha mkuu’. ‘Tumefikia mafanikio mazuri msimu uliopita na kuweka historia katika klabu hii kubwa. Dhumuni letu ni kuendelea kutengeneza hilo’.

Chanzo: Mpiratz