Diva na Diamond

Baada ya jana kuachia rasmi wimbo wake ‘Piga Simu’ uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu, mtangazaji/mwimbaji Loveness aka Diva ameeleza sababu za kwanini sauti yake inafanana na Rehema Chalamila aka Ray C kwenye wimbo huo.

Akiongea na kipindi cha XXL, Diva amesema sauti yake ndivyo inavyosikika siku zote aimbapo na ni kwasababu yeye anatokea Tanga ambako wanawake wengi wana sauti hizo (???).

Ameongeza kuwa maneno ya wimbo wa Ray C ‘Uko wapi’ ameyatumia kwasababu mara nyingi huyatamka kwa mpenzi wake ambaye muda mwingi ni mtu wa mishemishe na safari za nje ya nchi.

Akiongea kwa ‘mbwembwe’ na kujiamini kama kawaida yake, Diva amesema ubusy wa mpenzi wake ndio ulimfanya aandike wimbo huo kwakuwa mara nyingi hupenda mpenzi wake ampigie simu ili kumpunguzia upweke wa kuwa mbali naye.

Katika hatua nyingine Diva amemtaja mtunzi msaidizi wa wimbo huo aliomshirikisha Diamond kuwa ni mtangazaji mwenzie wa Clouds FM, Soud Brown aka Gossip Cop.

Aliongeza kuwa wimbo huo waliurekodi usiku kucha na Diamond huku akisema ilikuwa rahisi kwa mzee wa ‘Mawazo’ kumkubalia collabo ya bure kwakuwa yeye ni ‘diva’ na radio personality!!!

Amesema mashabiki wake wategemee wimbo mwingine uitwao ‘Mgonjwa kwa raha zako’ hivi karibuni na kudai kuwa pamoja na kuingia rasmi kwa game la muziki hawezi kuacha utangazaji kwakuwa anakipenda mno kipindi chake.

source;bongo5