Moto mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza zaidi maduka 10 eneo la Miyomboni katika Manispaa ya Iringa usiku huu.

Moto huo ambao chanzo chake bado kufahamika umezuka majira ya saa 2 usiku wa kuamkia leo katika eneo hilo la Uhindini kata ya Miyomboni mjini Iringa.

Baadhi ya wafanyabiashara waliokumbwa na tukio hilo la moto kuteketeza maduka yaowamesema kuwa moto huo ulianza katika chumba kimoja wapo cha duka na kuwa wanahisi ni hitirafu ya umeme.

Hata hivyo wamesema kuwa baada ya moto huo kuanza kuwaka walipata ushirikiano kutoka kwa kikosi cha zima moto Manispaa ya Iringa ambao walifika kwa wakati na kuishiwa maji kabla ya kuuzima moto huo.

Pia walisema wakati gari la zima moto limekwenda kuchota maji mto Ruaha vibaka walitumia nafasi hiyo kupora mali mbali mbali na kujikuta wakiishia katika mikono ya polisi ambao walitanda eneo hilo.

Diwani wa kata ya Miyombini kitanzini Jesca Msambatavangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo pamoja na kukipongeza kikosi cha Zimamoto mjini Iringa kwa kufika kwa wakati eneo la tukio huku akiwataka wananchi kuacha kulaumu kikosi hicho kwa kazi kubwa waliyoifanya.

source:francisgodwin.