KITIMTIMU cha aina yake kilitokea katika gesti maarufu iliyopo Mbuyuni Kunduchi-Mtongani jijini Dar es Salam kufuatia njemba mmoja kudakwa akiwa na mke wa mtu wakiigaragaza amri ya sita ya Mungu, Amani lina ishu mkononi.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio, ishu hiyo ilijiri hivi karibuni mishale ya saa 3:30 usiku katika gesti hiyo.
Shuhuda akasema mfumaniaji ambaye ni mwenye mke (jina tunalo) alifanikisha kuwanasa wawili hao baada ya kuwafuatilia kwa muda mrefu toka aliposikia penzi lake linasalitiwa.
Ikadaiwa kuwa siku ya tukio, mume alianza kuingiwa na shaka saa 1:00 usiku baada ya mkewe kuonekana yuko kwenye harakati za kujiandaa kwa ajili ya mtoko ambao hakuwa na taarifa nao na alipomuuliza alisema anakwenda kumjulia hali mtoto wa rafiki yake aliyekuwa anaumwa.
Ndipo mume huyo machale yakamcheza, akajipanga kwa kumpigia simu dereva wa ‘bodaboda’ na kumpa kazi ya kumfuatilia mkewe kila atakapotia mguu kisha amtaarifu kwa simu.
Shuhuda akasema: “Baada ya mke kujikwatua vilivyo, akatoka nje bila kufahamu kinachoendelea, akakodi pikipiki ileile ambayo ilikuwa ikimsubiri atoke halafu imfuatilie na hivyo kurahisisha kazi ya dereva.
“Alipoondoka tu, mumewe akachukua pikipiki nyingine na kumpitia mpigapicha ili apate ushahidi kwa kile ambacho atakishuhudia.
“Bahati nzuri nyingine, mbele mwanaume alikutana na askari wa doria na kuwaeleza dukuduku lake, ndipo nao wakaamua kumsaidia kwa ajili ya usalama zaidi,” alisema shuhuda huyo.
Kwa upande wake, mume naye alisema baada ya mkewe kuondoka, dereva wa pikipiki alimjulisha kuwa mkewe alimfikisha Mbuyuni, lakini alichukuliwa na jamaa mmoja kwenye gari wakaelekea maeneo ilipo gesti hiyo.
Alisema: “Baadaye dereva huyo wa bodaboda aliniambia kuwa mke wangu na huyo jamaa wamezama ndani ya gesti hiyo ambayo haikuwa mbali sana na maeneo hayo ya Mbuyuni, tena wapo chumba namba sita. Da! Inauma sana.”
Akasema ndipo yeye na ‘manjagu’ wakazama hapo kisha kugonga chumba hicho na kumkuta mkewe akiwa amejifunga shuka la gesti hiyo na jamaa akiwa anajiandaa kuvua nguo, tayari kwa ‘kubanjuka’.
Hata hivyo, shauri hilo liliishia hapohapo baada ya jamaa kujitetea kuwa hakujua kama mwanamke huyo ni mke wa mtu kwani hata mwanamke naye hakumtaarifu kwamba ameolewa.
Mpaka gazeti hili linakatiza mitamboni, haikujulikana ni hatua gani mume huyo alikwenda kuzichukua kwa mkewe baada ya kubaini kuwa alimficha ukweli.

globalpublishers