Raisi wa Malawi Joyce Banda


Rais wa Malawi Joyce Banda ambae ni rais wa pili mwanamke Afrika, amepongezwa kwa uamuzi wa kuiuza ndege iliyokua inatumiwa na aliyekua rais wan chi hiyo Marehemu Bingu wa Mutharika pamoja na magari 60 ya kifahari aina ya Mercedes benz ili kuchangisha fedha zitakazosaidia watu mbalimbali wanaoumia na umasikini nchini humo.

Kwa mujibu wa Africa Review Vyombo hivyo vya usafiri vinakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 15 za kimarekani fedha ambazo Rais Joyce Banda amesema zitatumika kununua dawa za hospitali, maji safi, madaktari, kulipa wafanyakazi wa serikali na mahitaji mengine ya muhimu ya nchi.