Harry Redknapp

Uongozi wa Redknapp, Tottenham umeisha baada ya klabu hiyo kutangaza kumuondoa kocha huyo.  David Moyes na Roberto Martinez ndio wanachuana kuchukua nafasi hiyo baada ya kushikiliwa kwa miaka mitatu na nusu na Redknapp.

Baada ya juhudi za muda mrefu za kutaka kumuondoa kocha huyu, Redknapp alisimama kidete kutetea nafasi yake hiyo. Mwenyekiti wa bodi, Bwana Daniel Levy alisema, ‘Uamuzi huu haujachukuliwa kirahisi. Harry alikuja katika kipindi ambacho uzoefu wake na msaada wake ulihitajika.’

‘Uamuzi huu haushushi kazi ya Harry aliyoifanya kwa kipindi chake na ninamshukuru kwa mchango wake mkubwa aliotoa’. ‘Harry ataendelea kukaribishwa Lane’.

Redknapp alisema, ‘Nimefurahia muda wangu Spurs na ninajivunia mafaniko yangu’. ‘Nina huzuni kuondoka, lakini nataka kuwashukuru wachezaji, wafanyakazi na mashabiki wote kwa sapoti yao walionipa kipindi chote hiki’.

Chanzo: Mpiratz