Zaidi ya Abiria 20 wa Basi wakiwemo wanafunzi wa shule wamenusurika kupoteza maisha eneo la Maziwa Ituta mapema leo asubuhi katika ajali iliyohusianisha magari matatu.


Mashuhuda wa tukio hilo wamesema abiria wote walikuwepo kwenye basi la Abiria aina ya Hiace walikuwa wakitokea Mwanjelwa kwenda Mbalizi katika barabara ya Mbeya- Zambia wamejuruhiwa na wamekimbizwa hospitali ya Rufaa.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:20 asubuhi.

Wameongeza kusema Dereva wa Hiace hiyo ambaye naye amejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo amefikishwa hospitalini akiwa hoi bin taaban alikuwa anataka ku-over take Lori lililokuwa limeegeshwa pembeni ndipo Lori jingine lililokuwa kasi likitokea Zambia likaziba barabara hivyo fursa iliyokuwepo kwa wakati huo ni kulivaa Lori lililokuwa limeegeshwa.

Maafisa wa Jeshi Polisi walifika eneo la tukio na kuwasaidia majeruhi wa ajali hiyo ambayo ni juma moja limepita tangu ajali nyingine ya basi la Abiria kutokea maeneo ya Itangano, Ijombe Igawilo Jijini Mbeya majira ya mchana wa Jumatano ya Juni 7 mwaka huu ambayo iliua abiria 13 na wengine 23 kujeruhiwa

jaizmelaleo